Ukuzaji wa taaluma ya ualimu umerahisishwa
Walimu ndio weledi zaidi katika kuwafundisha wanafunzi. Faved ni huduma isiyolipishwa inayowasaidia walimu kubadilishana mawazo na kuwaimarisha wanafunzi kimasomo kwa kushiriki mbinu ambazo zimejaribiwa na kutathminiwa darasani kote ulimwenguni.
Faved ilipokea Tuzo la Promising Innovation Award kwenye warsha ya Jacobs Foundation MIT Solveathon mnamo Juni 2021. Huduma hii iliyoundwa na HundrED na Schools2030, sasa inapatikana kwenye simu za mkononi na inaendelezwa kwa ushirikiano na walimu wanaoshiriki katika mpango wa Schools2030. Pakua kutoka kwenye Google Play Store na App Store.