mchezo wa bao kuondoa tatizo la kugawanya shuleni
په Numeracy
Bao ni mchezo wa asili ambao huchezwa na jamii inayowazunguka wanafunzi na wengi wao hucheza mchezo huo.kwahiyo kupitia bao hili mwanafunzi atakuwa na uwezo wa kujifunza kugawanya hata akiwa peke yake au na mwanafunzi mwenzake kwa njia ya kucheza bao hili
bao lina sehemu nne.sehemu ya kwanza ni chumba cha kuhifadhia kete zote za kuchezea.sehemu ya pili ni sehemu kwa ajili ya kete zinazowakilisha namba inayogawanywa.sehemu hii ina maeneo matatu ambayo inawakilisha thamani ya tarakimu katika namba yaani mamoja,makumi na mamia.sehemu ya tatu ni eneo linalokaa kete zinazowakilisha namba ya kugawanyia na sehemu ya nne ni eneo kwa ajili ya kuweka kete za majibu.sehemu hii pia ina maeneo matatu yanayowakilisha thamani ya tarakimu katika namba yaani mamoja,makumi na mamia
Weka kete katika sehemu ya kwanza yaani eneo zinapokaa kete zote za mchezo
Weka kete katika sehemu ya pili yaani eneo zinapokaa kete zinazowakilisha namba zinazogawanywa.mfano umepewa namba 396 ÷ 3= utwaweka kete 6 eneo la mamoja,kete 9 eneo la makumi na kete 3 eneo la mamia kuwakilisha 396.
Weka kete sehemu ya tatu yaani eneo zinazokaa kete zinazowakilisha namba za kugawanyia.mfano 396÷3=kete tatu huzo zitawakilisha namba 3 iliyopo kulia mwa alama ya kugawanya ÷
Ondoa kete 3 katika chumba cha namba zinazogawanywa katika eneo la mamia.Idadi ya matendo ya kuondoa kete 3 ndiyo jibu la mamia 3÷ 3= 1 kwahiyo wwka kete moja katika sehemu ya kuweka majibu eneo la mamia.Fanua hivo kwa namba zote zinazoendelea
Kama kete zilizopo sehemu ya kete zinazogawanywa eneo la mamia ni chache kuliko zile za kugawanya hamisha kate hizo kwa makumi.mfano 192÷2= 1 ni ndogo kuliko 2 hivyo ifanye 1 kuwa makumi ambapo itakuwa ni sawa na 10 kisha peleka kete 10 kwenye eneo lenye kete 9 kwahiyo katika eneo hilo kutakuwa na kete 19.kete 19 ukiondoa mafungu ya kete mbilimbili utaondoa mafungu 9 na kete moja itabaki.Badili tena kete 1 kuwa makumi ambpo itakuwa ni sawa na 10 kisha hamishia kete kumi katika eneo la makumi ambamo kuna kete 2 kwahiyo kete zitaongezeka na kuwa kete 12.Endelea kutoa mafungu ya kete mbilimbili.