Hazina ya Maneno ili Kupanua Akiba ya Msamiati kwa Mtoto
katika Kusoma na kuandika
Kategoria ndogo na maneno maalum
Jinsi ya kupanua akiba ya msamiati kwa mtoto kwa njia ya kufurahisha na ya kuvutia Katika zoezi hili, unashirikiana na mtoto wa miaka 4–8 kuunda 'hazina ya maneno' na kwa pamoja mnajifunza jinsi ya kutumia maneno mapya kwa ubunifu.
Anza kwa kutafuta maneno ya kuongeza kwenye hazina. Unaweza kutafuta maneno katika vitabu vya hadithi, magazeti, vitabu vya maombi, brosha, vitu vyenye lebo, au kalenda. Mtu mmoja anaweza hata kumsomea mwingine kitabu ili kupata maneno ya kuweka kwenye hazina ya maneno.
Kila mtu anapaswa kuchagua maneno matatu. Maneno yanaweza kuwa yenye ugumu wa viwango mbalimbali, yote yanaanza kwa sauti sawa, yote yana idadi fulani ya herufi, au yahusiana na mada fulani. Huenda baadhi ya maneno uliyochagua yakawa magumu kwa mtoto.
Andika kila neno kwenye karatasi au kadibodi yake.
Weka karatasi zote kwenye chupa au kontena – hii ni chupa ya maneno ya familia.
Kila siku chagua neno jipya kutoka kwenye chupa. Tafuta neno au jadili maana yake.
Fanya zoezi la kusoma neno hilo kwa sauti. Tunga vifungu vya maneno au sentensi fupi kwa kutumia neno hilo. Simulia hadithi kwa kutumia maneno hayo. Tafsiri neno katika lugha nyingine. Imba wimbo unaohusiana na neno hilo. Igiza neno. Tafuta maneno mengine yenye urari, kwa mfano, samba, bamba, pamba nk.
Rudisha maneno kwenye chupa ili myasome tena baada ya siku chache na mjaribu kukumbuka.
BONASI: Chora picha ya neno. Inaweza kuwa mchoro wa kawaida au wa kina. Vinginevyo, toa maneno yote kwenye chupa na utunge hadithi kwa kutumia maneno hayo. Simulia au igiza hadithi. Mnaweza kufanya hivi kama kikundi kimoja kikubwa au vikundi vidogo na kuona ni nani anayeweza kutunga hadithi ya kuchekesha au ya ubunifu zaidi kwa kutumia maneno. Furahia!