ujifunzaji wa masomo nje ya darasa (michezo)
katika Numeracy
Mbinu imebuniwa na
Winfrida Komba
Kategoria ndogo na maneno maalum
Imeshirikiwa kwenye Faved na
Wanafunzi kutokuwa makini darasani kwa kuwaza michezo. Wanafunzi wanaenda kujifunza huku wakiwa wanacheza michezo wanaocheza kila siku
Maagizo ya hatua kwa hatua kwa walimu wengine
1.kutambua michezo wanayoipenda na kucheza muda wote wanafunzi wakiwa shuleni na nyumbani
2. Baada ya kuitambua unaenda kuibadili na kuona namna watakavyokuwa wanacheza huku wakijufunza
3. Baada ya hayo utaingia darasani kufundisha mada kama kawaida na zana baada ya kumaliza maada. Wanafunzi watenda kufanya marudio ya mada hiyo uwanjani huku wakiwa wanacheza michezo
4. Mfano wa michezo hiyo ni mpira wa miguu,handball,rede na kuruka kamba
Je, unatarajia matokeo yapi?
1.wanafunzi wanafurahia ujifunzaji wakiwa nje ya darasa.
2.imeongeza umakini katika ujifunzaji
3.wanafunzi wanajifunza kwa ushindani
4.somo linaelewaka kwa urahisi
5.wanafunzi wanajifunza huku wakiwa wanacheza
6.imewajengea kuwa na kumbukumbu ya muda mrefu
7.imeongeza mahudhurio ya wanafunzi
TOA MAONI