Kugusa na Kuhisi
katika Ustawi wa Kihisia
Kutumia hisia za watoto kutambua vitu kulingana na umbo na ulaini.
Funika kisanduku cha kadibodi ukitumia karatasi nyeupe, kiwe na tundu ambalo mtoto anaweza kuingiza mkono.
Mweleze mtoto apambe kisanduku apendavyo kwa kutumia picha na mapambo.
Baada ya kukitengeneza atakavyo, weka vitu kadhaa kwenye kisanduku lakini usimweleze wala usimwonyeshe mtoto vitu hivyo. Kwa mfano, weka ndizi, kitabu, penseli, jiwe nk.
Mwambie mtoto aweke mkono wake ndani ya kisanduku na aguse kitu. Mpe muda wa kutosha wa kugusa na kuhisi kilicho kwenye kisanduku, kwa kuwa mchezo huu unawahimiza kutumia hisia zingine kando na kutazama.
Mweleze afafanue kitu alichogusa na ataje jina lake kabla ya kukitoa ili kuona ikiwa amepata.
Muulize maswali kama, je kitu hicho ni laini au gumu? Je, ni umbo gani? Je, ni ngumu au laini? Unafikiri ni nini? Unajuaje?