Kutumia hisia za watoto kutambua vitu kulingana na umbo na ulaini.
Kupima umbali kwa kutumia vitu tofauti, na kulinganisha na kupanga umbali kuanzia fupi hadi ndefu zaidi. Husaidia kukuza ubunifu na uwezo wa kufikiria.
Zoezi hili linalenga kuboresha utambuzi wa nambari, na usawazishaji wa upande wa kulia na wa kushoto katika hali mbalimbali.
Kutambua njia mbalimbali za kuonyesha wema.
Kuainisha vitu katika vikundi kulingana na sifa zao tofauti. Hii husaidia katika ustadi wa kufanya maamuzi wakati wa kuchagua vitu na picha. Pia husaidia kukuza ubunifu na uwezo wa watoto kufikiria wanapoamua jinsi ya kuunda na kupamba vitabu vyao vya picha
Kuelezea kuhusu eneo kwa kutambua vitu muhimu na kutumia michoro kuonyesha eneo lilivyo. Hii husaidia watoto kuelewa waliomo katika jamii yao wanapojifunza kuhusu vitu na maeneo muhimu mahali walipo.
Kukimbia na kurukaruka nje ili kuchochea siha, kushirikiana, kustahilimi, uwiano na kufahamu mazingira. Husaidia pia kukuza ustadi wa kutatua matatizo na kuwaza kwa makini.
Kulinganisha na kuweka katika vikundi, husaidia katika utambuzi wa nambari, umakinifu na kumbukizi.
Jinsi ya kuelezea dhana dhahania kama vile wakati, kwa watoto wenye umri wa miaka 9-13? Katika zoezi hili, watoto huelewa dhana ya wakati kwa kuchora vivuli vya vitu tofauti.
Kufanya mazoezi ya kupiga makofi ili kuboresha ujuzi wa kuoanisha macho na mikono, na kuanzisha na kufuata midundo na mifululizo. Husaidia kukuza uwezo wa mawasiliano na ushirikiano kwa kupiga makofi na kukariri midundo.
Kujifunza jinsi ya kutoa na kufuata maagizo yaliyotolewa na wanakikundi/kiongozi wa kikundi.
Kufahamu kuhusu usawazisho na uzani, ikiwemo kutumia macho na mikono kwa pamoja.
Mashine ya Mawimbi huwasaidia wanafunzi kuelezea kuhusu mwendo wa mawimbi. Pia huwawezesha kubaini uhusiano kati ya urefu wa kitu na urefu wa mawimbi. Kupitia zoezi hili, wanafunzi pia hukuza ubunifu na ustadi wa kufikiria.
Uwezo wa kutambua nambari na kujumlisha kwa kuzingatia mawasiliano, kufanya kazi pamoja, na ushirikiano.