Kuongeza kwa Kutumia Sahani
katika Stadi za Kijamii
Uwezo wa kutambua nambari na kujumlisha kwa kuzingatia mawasiliano, kufanya kazi pamoja, na ushirikiano.
Maagizo ya hatua kwa hatua kwa walimu wengine
Watoto waandike nambari 1-20 kwenye sahani 20 za karatasi.
Wagawanye watoto katika vikundi.
Kila mtoto achague sahani 4 za karatasi na azishikilie.
Mtu mzima ataje nambari kisha watoto wajigawanye katika vikundi kulingana na jinsi wanavyoweza kupanga nambari zilizoandikwa kwenye sahani zao katika hisabati ya kuongeza ambayo matokeo yake ni nambari iliyotajwa.
Mfano: 11 ikitajwa, watoto walio na nambari 6 na 5 wanaunda kikundi kwa sababu 6 + 5 = 11.
TOA MAONI