Kufanya mazoezi ya maneno na vifungu vya maneno mapya katika hali tofauti na kueleza maana ya maneno au vifungu vya maneno kwa kutumia vitendo mwafaka. Husaidia katika kusikiliza kwa makini na kujibu ipasavyo.
Uwezo wa kutambua nambari na kujumlisha kwa kuzingatia mawasiliano, kufanya kazi pamoja, na ushirikiano.
Kuelezea kuhusu eneo kwa kutambua vitu muhimu na kutumia michoro kuonyesha eneo lilivyo. Hii husaidia watoto kuelewa waliomo katika jamii yao wanapojifunza kuhusu vitu na maeneo muhimu mahali walipo.
Jinsi ya kuelezea dhana dhahania kama vile wakati, kwa watoto wenye umri wa miaka 9-13? Katika zoezi hili, watoto huelewa dhana ya wakati kwa kuchora vivuli vya vitu tofauti.
Kupima umbali kwa kutumia vitu tofauti, na kulinganisha na kupanga umbali kuanzia fupi hadi ndefu zaidi. Husaidia kukuza ubunifu na uwezo wa kufikiria.
Kujifunza jinsi ya kutoa na kufuata maagizo yaliyotolewa na wanakikundi/kiongozi wa kikundi.