Cookie preferences

Faved uses cookies to enhance user experiences, to personalise content, and analyse our web traffic. By clicking "Accept all" you agree to the use of all cookies, including marketing cookies that may help us deliver personalised marketing content to users. By selecting "Accept necessary" only essential cookies, such as those needed for basic functionality and internal analytics, will be enabled.
For more details, please review our Cookie Policy.
Accept all
Accept necessary

Maigizo

katika Kusoma na kuandika

verified Verified practice
Mbinu imebuniwa na Faved Organisation
F
visibility 39
favorite_border 1
favorite_border Mbinu unayopenda

Kategoria ndogo na maneno maalum

Imeshirikiwa kwenye Faved na

Maelezo

Kufanya mazoezi ya maneno na vifungu vya maneno mapya katika hali tofauti na kueleza maana ya maneno au vifungu vya maneno kwa kutumia vitendo mwafaka. Husaidia katika kusikiliza kwa makini na kujibu ipasavyo.

Maagizo ya hatua kwa hatua kwa walimu wengine

Unda orodha ya vitu, watu, au maeneo yanayoweza kuigizwa. Andika kila kipengee kwenye kadi yake. Hakikisha ni maneno ambayo mtoto anaweza kusoma na tayari anayafahamu, au unaweza kuchora kitu hicho badala ya kukiandika (e.g., kupiga mswaki, kuamka, kusoma kitabu, kucheza densi, ndizi, ndege, nyoka, mbwa n.k.) Yaweke kwenye kisanduku au begi.

Mtoto mmoja anachagua kadi na haonyeshi mtu mwingine yeyote. Mtoto huyu anaigiza neno lililo kwenye kadi ili wengine wajaribu kukisia neno hilo. Mtoto anapaswa kuigiza neno hilo bila kutamka chochote, ndani ya muda uliowekwa.

Kabla ya kuigiza neno, mtoto anaweza kuwajulisha wengine kategoria ya neno au kifungu cha maneno na idadi ya maneno yaliyomo. Kwa vyovyote vile, lazima afanye hivi bila kuzungumza.

Kategoria: Kuiga uimbaji ikiwa ni wimbo. Kuiga kitendo kinachohusu kamera ikiwa ni filamu. Kuiga kitendo kinachohusu kitabu ikiwa ni jina la kitabu, nk.

Idadi ya maneno: Onyesha idadi kwa vidole (e.g., ikiwa kifungu ni “kucheza kandanda” inua vidole viwili). Atakayekisia neno au kifungu kwa usahihi ndiye atakayechukua kadi na kurudia mchezo.

Husisha watu wote hadi kila mtu apate fursa ya kuchagua kadi. Ikiwa unacheza na watoto kadhaa, wagawanye katika vikundi viwili vinavyotoshana. Mchezaji wa kikundi cha kwanza anachora kadi na wanakikundi wenzake wanajaribu kukisia jibu kabla ya muda kuisha. Kisha mwanakikundi wa upande wa pili anachora kadi na wenzake wanajaribu kukisia jibu kabla ya muda kuisha.

Mchezo huendelea hadi kadi zikwishe au hadi kila mchezaji awe atakapopata fursa sawa. Hesabu ni kadi ngapi wahusika walipata usahihi ndani ya muda uliowekwa. Hayo ndio matokeo.

TOA MAONI

Fave mazoezi ili kuweza kujiunga na majadiliano na kutoa maoni favorite_border Shiriki kwenye Faved