Kutambua njia mbalimbali za kuonyesha wema.
Kuelezea kuhusu eneo kwa kutambua vitu muhimu na kutumia michoro kuonyesha eneo lilivyo. Hii husaidia watoto kuelewa waliomo katika jamii yao wanapojifunza kuhusu vitu na maeneo muhimu mahali walipo.
Jinsi ya kuelezea dhana dhahania kama vile wakati, kwa watoto wenye umri wa miaka 9-13? Katika zoezi hili, watoto huelewa dhana ya wakati kwa kuchora vivuli vya vitu tofauti.
Mashine ya Mawimbi huwasaidia wanafunzi kuelezea kuhusu mwendo wa mawimbi. Pia huwawezesha kubaini uhusiano kati ya urefu wa kitu na urefu wa mawimbi. Kupitia zoezi hili, wanafunzi pia hukuza ubunifu na ustadi wa kufikiria.
Kuainisha vitu katika vikundi kulingana na sifa zao tofauti. Hii husaidia katika ustadi wa kufanya maamuzi wakati wa kuchagua vitu na picha. Pia husaidia kukuza ubunifu na uwezo wa watoto kufikiria wanapoamua jinsi ya kuunda na kupamba vitabu vyao vya picha
Kukimbia na kurukaruka nje ili kuchochea siha, kushirikiana, kustahilimi, uwiano na kufahamu mazingira. Husaidia pia kukuza ustadi wa kutatua matatizo na kuwaza kwa makini.
Kufanya mazoezi ya maneno na vifungu vya maneno mapya katika hali tofauti na kueleza maana ya maneno au vifungu vya maneno kwa kutumia vitendo mwafaka. Husaidia katika kusikiliza kwa makini na kujibu ipasavyo.
Jiandae kufafanua neno 'habari bandia' darasani unapoanza somo lako. Habari bandia ni taarifa za uwongo au za kupotosha zinazowasilishwa kama habari. Taarifa za uwongo mara nyingi huwa na lengo la kuharibu sifa ya mtu au shirika, au kupata pesa kupitia mapato ya utangazaji.