Kuhusu Ulimwengu Wangu
katika Sanaa na Ubunifu
Kategoria ndogo na maneno maalum
Kuainisha vitu katika vikundi kulingana na sifa zao tofauti. Hii husaidia katika ustadi wa kufanya maamuzi wakati wa kuchagua vitu na picha. Pia husaidia kukuza ubunifu na uwezo wa watoto kufikiria wanapoamua jinsi ya kuunda na kupamba vitabu vyao vya picha
Mtoto huchagua mada/maudhui anayopenda na angependa kushiriki na wengine. Msaidie mtoto kutengeneza kitabu cha picha kwa kutumia daftari tupu au karatasi iliyotengenezwa upya.
Tafuta vitu au picha zinazohusiana na mada/maudhui kwenye magazeti au majarida. - Mifano ya vitu: manyoya, majani, mawe, vitu vinavyopatikana nyumbani au kwa urahisi vinavyoweza kubandikwa kwenye kitabu cha picha - Mifano ya picha: kutoka kwenye gazeti, majarida, vitabu vya zamani, au brosha.
Kata picha kisha upachike vitu na picha kwenye kitabu cha picha kwa kutumia gundi.
Pamba kurasa, k.m., tumia michoro au picha, ongeza maneno au vifungu vya maneno. Zungumzia kuhusu yaliyomo kwenye kitabu cha picha na sababu ya mtoto wako kuchagua vitu hivi.
Mhimize mtoto wako kuonyesha kitabu chake cha picha kwa marafiki, majirani na familia.
Mtoto anaweza kuandika jina lake kwenye jalada la kitabu cha picha ili kuonyesha ni chake.