Kusimama Ulipo Unapoguswa
katika Afya na Lishe
Kategoria ndogo na maneno maalum
Kukimbia na kurukaruka nje ili kuchochea siha, kushirikiana, kustahilimi, uwiano na kufahamu mazingira. Husaidia pia kukuza ustadi wa kutatua matatizo na kuwaza kwa makini.
Teua mtoto atakayekuwa "mlengaji" (anayekimbia na kugusa wengine).
Baini sehemu ambako watoto hawastahili kufika. Hii itawezesha watoto kucheza sehemu mahususi.
Mtoto wa "mlengaji" anapaswa kufunga macho kisha kuhesabu hadi 10. Wakati huu, watoto wengine wanakimbia na kujificha.
Mtoto "mlengaji" anapomaliza kuhesabu, anafungua macho na kukimbia huku na huko akiwatafuta wengine na kuwagusa.
Anapaswa kuwagusa mkono, bega au mgongo. Watoto wanaweza kukimbia wakifuatwa ili wasiguswe. "Mlengaji" anapomgusa mtoto mwingine, aliyeguswa anapaswa kusimama aliko kana kwamba "amegandishwa".
Mchezo huisha wakati kila mtu ameganda. Mtu wa mwisho kuguswa ndiye huwa "mlengaji" katika awamu inayofuata.