Cookie preferences

Faved uses necessary cookies that are essential to use the service and for us to provide a better user experience. Read more about our cookies.
Accept cookies

Mashine ya Mawimbi

katika Sayansi

Maelezo

Mashine ya Mawimbi huwasaidia wanafunzi kuelezea kuhusu mwendo wa mawimbi. Pia huwawezesha kubaini uhusiano kati ya urefu wa kitu na urefu wa mawimbi. Kupitia zoezi hili, wanafunzi pia hukuza ubunifu na ustadi wa kufikiria.

Maagizo ya hatua kwa hatua kwa walimu wengine

Msaidie mtoto wako kutayarisha mirija 20, klipu 40 za karatasi, na vipande 2 virefu vya tepu.

Weka chini kipande kirefu cha tepu, upande wenye gundi ukiangalia juu.

Chora mstari katikati ya tepu ukitumia kalamu au kalamu ya wino. Pawe na nafasi sawa kati ya mstari mmoja na mwingine, yaani sentimita 4.

Kisha mtoto abandike mirija kwenye mistari hiyo ikifuatana, yote ikielekea upande mmoja. Hii ina maana kwamba mirija inapaswa kuwa wima kwenye tepu, na idadi ya mirija iwe sawa kila upande.

Fanya hili kuanzia juu hadi chini kwenye tepu hadi mirija yote ibandikwe.

Bandika ncha za pande zote mbili kwenye kiti. Urefu wa nafasi kati ya viti hivyo viwili unategemea urefu wa tepu. Weka kitu kizito juu ya ncha za tepu ili isianguke.

Gusa kidogo ncha moja ya mirija ili uone mawimbi kwenye tepu.

Jaribu kwa kugusa sehemu tofauti-tofauti au kwa uzito tofauti. Jadili jinsi hii inavyobadilisha urefu au kasi ya mawimbi.

Je, unatarajia matokeo yapi?

Matokeo

Ikiwa zoezi hili ni rahisi sana, unaweza kurekebisha kwa kuongeza uzito. Kwa mfano, ongeza uzani sawa pande zote. Kwa mfano, tafuta champali nzee zilizotumika kisha ukate vipande vidogo mviringo vinavyotoshana, au tumia vipande vya udongo vinavyotoshana. Je, hii inabadilishaje mashine ya mawimbi? Je, ukipunguza uzani, mawimbi yanabadilika vipi?
TOA MAONI

Fave mazoezi ili kuweza kujiunga na majadiliano na kutoa maoni favorite_border Shiriki kwenye Faved