Kuchora Kivuli
katika Sayansi
Jinsi ya kuelezea dhana dhahania kama vile wakati, kwa watoto wenye umri wa miaka 9-13? Katika zoezi hili, watoto huelewa dhana ya wakati kwa kuchora vivuli vya vitu tofauti.
Mtoto atafute kitu chochote ambacho angependa kuchora.
Weka kitu hicho kwenye karatasi tupu palipo na mwangaza wa jua. Waelekeze watoto wasogeze kitu hicho hadi waone kivuli kwenye karatasi. Je, unaona kivuli? Ikiwa ndiyo, chora. Ikiwa sivyo, kwa nini? Jaribu kusogeza karatasi na kitu hicho mahali pengine ili uone kivuli.
Kwa kutumia kalamu au penseli, waombe watoto wachore muundo wa kivuli cha kitu hicho.
Waelezee watoto maana ya urefu na mkao wa kivuli, na jinsi zinavyoonyesha wakati na uwiano kati ya jua na kitu hicho.
Rudia zoezi hilo nyakati tofauti za siku ili kuelewa jinsi wakati huathiri vivuli.
Zoezi la ziada: Watoto wanaweza kupamba vivuli kwa kutumia rangi.
Zoezi la ziada: Rudia zoezi hilo kwa kutumia mwangaza wa tochi badala ya jua. Jaribu kusogeza tochi karibu au mbali na kitu hicho. Je, kubadilisha mkao wa tochi na umbali wake kunabadilishaje kivuli? Je, kinakuwa ndogo? Kubwa zaidi? Kirefu zaidi? Kifupi zaidi? Simamisha tochi mahali ili mtoto atumie mikono yote miwili kuchora kivuli.
Kando na karatasi: Unaweza kuchora kivuli ardhini kwa kutumia kijiti.