Njia ya ndege
katika Sanaa na Ubunifu
Kategoria ndogo na maneno maalum
Kupima umbali kwa kutumia vitu tofauti, na kulinganisha na kupanga umbali kuanzia fupi hadi ndefu zaidi. Husaidia kukuza ubunifu na uwezo wa kufikiria.
Tengeneza ndege moja ya karatasi kwa kila mtoto. Hakikisha watoto au vikundi havijakaribiana ili pawe na nafasi ya kutosha ya kupeperusha ndege zao.
Chora chini mstari unaoonekana. Hii ndiyo njia ya ndege ambapo watoto watapeperusha ndege zao.
Watoto wanapaswa kusimama nyuma ya mstari na kurusha ndege zao za karatasi kwelekea upande mmoja mbali zaidi kadri wawezavyo.
Baada ya ndege za karatasi kutua, watoto watabaini umbali ambao ndege zao zilitua kutoka kwenye njia ya ndege, k.m., kwa kupima hatua za nyayo.
Umbali unaweza kupimwa kwa kutumia kitu cha kawaida, k.m. rula/viatu, uzi.
Ndege itakayotua mbali zaidi kutoka kwenye njia ya ndege itashinda.