Waweke katika Vikundi vya Wawili Wawili
katika Kuhesabu
Kulinganisha na kuweka katika vikundi, husaidia katika utambuzi wa nambari, umakinifu na kumbukizi.
Kusanya vifuniko 20 vya chupa kisha uvigawe mara 2 ili kila kikundi kiwe na vifuniko 10. Andika nambari 0-9 ndani ya vifuniko katika kila kikundi. Hakikisha nambari 6 na 9 hazifanani.
Geuza vifuniko vya chupa chini ili nambari zisionekane kisha uchanganye vifuniko vyote pamoja. Zipange mraba ambapo vifuniko vinne viko upande na vitano kwenda juu.
Mweleze mtoto achukue vifuniko viwili. Ikiwa nambari kwenye vifuniko alivyochukua zinalingana, mtoto atasalia na vifuniko vyote viwili. Ikiwa nambari hazilingani, mtoto anarejesha vifuniko vyote viwili kwenye mraba nambari zikiwa chini.
Rudia hadi mtoto aoanishe vifuniko vyote.
Ikiwa pana wachezaji wawili au zaidi, wanapaswa kupishana kuchukua vifuniko. Mtoto akipata nambari zinazolingana, atasalia na vifuniko. Iwapo nambari hazilingani, mtoto anarejesha vifuniko kisha wa pili anacheza. Mshindi ni mchezaji atakayepata jozi nyingi za vifuniko mwishoni mwa mchezo.